Hallo!! Breaking News za Leo Soma kwenye Ubao wetu Mweusi
BREAKING NEWS ZA TAREHE 05/05/2017
AJALI DAR:
BREAKING
NEWS ZA TAREHE 04/05/2017
Watu 2 wamekufa, 1 ajeruhiwa baada ya Fuso la nyanya kutoka
Iringa kuligonga lori la Mchanga kwa nyuma eneo la Tabata Mwananchi, Polisi
wathibitisha.'
MAAFA TANGA:
Watu 2 wafa, 8 wajeruhiwa baada ya kutokea mafuriko kijijini
Magila, Kata ya Mkumbara, Korogwe, RPC Wakulyamba athibitisha. Tathmini
inafanyika.'
AJALI ARUSHA:
Wanafunzi na Walimu wa shule ya Lucky Vincent ya Arusha
wafariki baada ya gari lao kutumbukia Mto Malela wilayani Karatu. Taarifa zaidi
zitafuata.'
AJALI KARATU:
Polisi wathibitisha kuwa watoto 31 na walimu wamefariki
katika ajali iliyotokea katika Mto Malera.'
AJALI KARATU:
Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa RC wa Arusha
Mrisho Ganbo kufuatia vifo vya wanafunzi 32, Walimu 2 na dereva wa shule ya
Lucky Vicent.'
JPM ATEUA:
Rais John Magufuli amemteua Prof Egid Beatus Mubofu kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania "TBS" Ikulu yasema .'
VIWANGO FIFA:
Tanzania yabaki nafasi ya 135 katika msimamo wa viwango vya
FIFA uliotoka leo. Kenya yabaki 78 na Uganda 72. Brazil yaendelea kuongoza kwa
ubora.'
MATUMIZI YA EFD:
Meneja msaidizi Viwanja vya Leaders Club, Emmanuel Chacha
ashtakiwa kortini Kinondoni, Dar kwa makosa 2 ikiwemo kutotumia EFD kutolea
risiti.'
KOCHA MPYA:
Kocha Stuart Baxter ataondoka Supersport United mwishoni mwa
msimu na kujiunga na timu ya Taifa ya Afrika Kusini "Bafana
Bafana",SAFA yatangaza leo.'
BENITEZ MATATANI:
Kocha wa Newcastle Rafael Benitez ashtakiwa na FA kwa kutoa
maoni dhidi ya refa aliyechezesha mechi ya timu yake vs. Preston kabla ya
pambano.'
VITI MAALUM:
Catherine Ruge ameteuliwa kuwa mbunge Viti Maalum kupitia
Chadema, NEC yasema, Ruge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr Macha
aliyefariki Machi 31.'
BREAKING NEWS ZA TAREHE 03/05/2017
UBUNGE EALA:
Kamati kuu Chadema yateua watu 6 kugombea nafasi 2 za ubunge
wa Bunge la Afrika Mashariki, Tumaini Makene atangaza. Maisha,Wenje, Prof
Safari wamo .'
MAHOJIANO NA MAALIM:
Hakuna CUF-Lipumba wala CUF-Maalim bali maamuzi ya chama
yanafanywa na Baraza Kuu, asema Maalim Seif katika mahojiano kituo cha Clauds
TV.'
MAHOJIANO NA MAALIM:
Maalim Seif adai, kupitia Clauds TV, kuwa alijitoa kwenye
mazungumzo na Rais Shein baada ya tarehe ya marudio ya uchaguzi kutangazwa.'
MAHOJIANO NA MAALIM:
Maalim Seif asema kamwe hawezi kuketi meza moja ya
mazungumzo na Prof Lipumba kwa madai kuwa mwanasiasa huyo alikisaliti chama cha
CUF.'
MKONO WA MAALIM:
Nilifanya maksudi kutompa mkono Rais Shein kwa ili apate
ujumbe kuwa nilikasirika kuporwa haki yangu, asema Maalim Seif kupitia Clouds
TV.'
FAINALI FA:
Mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na
Mbao FC itachezwa katika Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, Rais wa TFF, Jamal
Malinzi atangaza.'
AJALI DAR:
Watu 2 wafa, 15 wajeruhiwa baada ya daladala kugongana na
lori jirani na duka Lifemate, Temeke, RPC Muroto asema. Miili yahifadhiwa
hospitalini Temeke.'
PEMBA MBARONI:
Polisi wa Tz, Uganda wanamchunguza Mtanzania Jack Pemba
aliyekamatiwa Entebe, nchini Uganda akituhumiwa kutakatisha fedha, Daily
Monitor laripoti.'
VYETI FEKI:
Waziri Kairuki asema bungeni, wanaodai kuonewa wakate rufaa
Utumishi, aonya adhabu zaidi kuwakabili wakishindwa kudhibitisha uhalali wa
vyeti vyao.'
BAJETI:
Waziri Ummy aomba Bunge lipitishe Sh1.16trn za Bajeti ya
Wizara ya Afya 2017/2018. Kamati yasema serikali haikutoa asilimia 50 ya fedha
2016/2017.'
UCHAGUZI KENYA:
Chama cha Jubilee chamtangaza mwanamuziki, Charles Njagua
"Jaguar" mshindi mchujo wa kupata nafasi kuwania ubunge wa jimbo la
Starehe, Nairobi.'
BREAKING NEWS ZA TAREHE 02/05/2017
MAJERAHA YA IBRA:
Straika wa Man United Zlatan Ibrahimovic amefanyiwa upasuaji
wa goti wenye mafanikio, atarajiwa kupona mapema, wakala wake Mino Raiola
asema.'
MDEE HATIANI:
Mbunge Halima Mdee akutwa na hatia ya kudharau mamlaka ya
spika, kutoa lugha ya matusi, kamati yasema. Yataka azuiwe kuhudhuria vikao
vilivyobaki.'
BULAYA HATIANI:
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya ameitwa hatiani kwa
kudharau mamlaka ya Spika, kamati ya Bunge yatangaza na kupendekeza na
kupendekeza apewe karipio kali.'
MBOWE HATIANI:
Kiongozi Kambi Rasmi ya upinzani, Freeman Mbowe akutwa na
hatia ya kudharau mamlaka ya spita,aomba radhi na kusamehewa, Kamati ya Maadili
yasema.'
UAMUZI WA BUNGE:
Bunge lawasamehe Freeman Mbowe na DC Mnyeti bila masharti
yoyote, Ester Bulaya kuandikiwa barua ya onyo huku Mdee akisamehewa kwa
masharti.'
KAMATI YA BUNGE:
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge yapendekeza DC
Alexander Mnyeti asamehewe baada ya kuomba radhi kutokana na kosa la kulidharau
Bunge.'
KESI YA WEMA:
Upelelezi wa kesi ya kukutwa na bangi
inayomkabili Miss Tz 2006, Wema Sepetu wakamilika, Korti ya Kisutu yaelezwa.
Kesi kuanza kusikiliz
0 Maoni :
Post a Comment