BREAKING NEWS ZA TAREHE 21/06/2017
PRINCE PHILIP ALAZWA:
Mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza , alazwa hospitali usiku wa kuamkia leo baada ya kupata maambukizo, Kasri ya Buckingham yaeleza
TAMKO LA BAVICHA:
Bavicha imesema itamfungulia kesi DC wa Ubungo Kisare Matiku ikidai amekiuka sheria kwa kuagiza Meya wa Ubungo nBoniface Jacob awekwe mahabusu.
ZIARA YA JPM:
ZIARA YA JPM:
Rais John Magufuli leo amemshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es salaam (Dawasa), Archard Mutalemwa astaafu
MAUAJI KIBITI:
Trafiki wawili wahofiwa kufa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Msafiri wilayani Kibiti, Kamanda Lyanga athibitisha
BREAKING NEWS ZA TAREHE 20/06/2017
TOHARA SIMIYU:
Zaidi ya wanaume 200 wilayani Bariadi wamefanyiwa tohara
bure katika kampeni ya upimaji maganjwa inayoendeshwa na Taasisi ya Islamic
Foundation.'
UCHAGUZI TFF:
BMT Limeitaka TFF Kuwaambia wagombea wa uchaguzi mkuu wa
shirikisho hilo kipengele kinachokataza kiongozi kuwa na kofia mbili katika
mchezo mmja.'
UCHAGUZI TFF:
Mgombea wa wa kiti cha urais wa TFF,Fredrick Masolwa
amerejesha fomu na kuahidi kubadilisha taswira ya shilikisho hilo
atakapochaguliwa Agosti 12.'
JAJI AJIUZULU:
Rais John Magufuli ameridhia ombi la kujiuzulu la Jaji wa
Mahakama Kuu Mwendwa Judith malecela kuanzia leo Ikulu yaeleza.'
RAIS APONGEZWA:
Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo amekutana na Rais
Magufuli Ikulu na kumpongeza kwa kuwa mfano bora Afrika kwa kutetea maslahi ya
nchi.'
MAGUFULI ZIARANI PWANI:
Rais John Magufuli awasili eneo la Bwawani-Kibaha Mkoa wa
Pwani kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.'
USAJILI:
Klabu ya Mbeya city imemsajili beki wa Kagera Sugar Erick
Kyaruzi Mopa kwa kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja na nusu.'
ZIARA YA JPM:
Rais Magufuli awataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo
vya dola kufichua wahalifu kibiti, adai uhalifu unachelewesha maendeleo
wilayani humo.'
SHABIKI AFARIKI:
Shabiki marufu wa yanga Ally Yanga amefariki dunia leo
katika ajali ya gari huko Mpwapwa,Dodoma,Kamanda Mambosasa athibitisha.'
BUNGENI DODOMA:
Spika wa Bunge Job Ndugai amemfukuza bungeni Mbunge wa jimbo
la Ukonga Mwita Waitara jioni hii Waitara aridhia na kutoka.'
TFF YAVUNA:
Shilikisho la soka Tanzania (TFF) limepata sh 18.4m kutoka
kwa wagombea 74 waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi
ujao.'
BUNGGENI DODOMA:
Bunge limepitisha Bajeti kuu ya serikari ya Mwaka wa Fedha
2017/2018 ya sh 31.7 trilioni jioni hii mjini Dodoma.'
RAMBIRAMBI:
Rais Magufuli ametuma rambirambi kwa familia na wanachama wa
ccm na uongozi wa klabu ya Yanga kutokana na kifo cha shabiki maarufu Ali
Yanga.'
SOKA:
katibi Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa asema Yanga haitaendelea
na kiungo Haruna Niyonzima huenda akajiunga simba.'
BREAKING NEWS ZA TAREHE 17/06/2017
MOTO URENO
Watu 57 wamekufa na wengine 59 wamejeruhiwa kwa moto
unaoendelea kuteketeza msitu nchini Ureno, mamlaka zathibitisha.'
SAKATA LA RONALDO
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amemuomba Christiano
Ronaldo abadili uamuzi wake wa kutaka kuachana na klabu hiyo.'
BREAKING NEWS ZA TAREHE 16/06/2017
MABAKI YA BABA WA NDUGAI
Wananchi wanaofukua mabaki ya mwili wa baba wa spika wa
Bunge Job Ndugai,Yustino Ndugai aliyezikwa Bukombe ili kuyapeleka Kongwa.'
KATIBA EPL
Ratiba ligi kuu England leo,mechi kuanzia Agosti 12ambapo
Chelse kuanza na Burnley, Man United vs West Ham,Arsernal vs Leicester.'
ATEKETEZWA GEITA
Mtu mmoja ameuawa kwa kuteketezwa kwa moto katika kitongoji
cha Afya wilayani Geita baada ya kutuhumiwa kuiba unga wa muhoho, polisi
wasema.'
UCHAGUZI TFF
Mbuge wa Ulyankulu,Peter Kaduru amechukua fomu ya kuwania
nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF, kupitia kanda ya Tabora na
Kigoma.'
HALI YA HEWA
Mamlaka ya hali ya Hewa nchini imetoa tahadhari ya kuwepo
upepo mkali na mawimbi makubwa baharini katika Mwambao wa Pwani Jumapili hii.'
MKATABA
Nahodha wa Simba, kiungo Jonas Mkud amesaini mkataba wa
miaka miwili wa kuendesha kuichezea klabu hiyo na kumaliza tetesi za kutaka
kujiunga na Yanga.'
0 Maoni :
Post a Comment