OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

BREAKING NEWS/HABARI ZA HIVI PUNDE PAGE 4

BREAKING NEWS ZA TAREHE 29/04/2017

HARAMBEE:
Zaidi ya sh200 milioni zimepatikana katika hafla ya kuichangia timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 "Serengeti Boys" iliyofanyika Dar.'

NUSU FAINALI SHIRIKISHO:
Simba yatinga fainali za kombe la shirikisho baada ya kuichapa Azam bao 1-0 Uwanja wa Taifa Dar, kesho ni Yanga vs Mbao FC, Mwanza.'

BREAKING NEWS ZA TAREHE 28/04/2017


UHAKIKI WA VYETI:
Rais Magufuli awasili katika ukumbi wa Chimwaga katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma.'

KESI YA OLE SABAYA:
Mahakama ya Arusha imeondoa kesi iliyokuwa inamkabili mwenyekiti wa UVCCM  Lengai Ole Sabaya kwa upande wa jamhuri kushindwa kuleta mashahidi.'

UHAKIKI WA VYETI:
Waziri Angela Kairuki asema uhakiki wa vyeti umebaini watumishi 9,932 wanatumia vyeti vya kugushi ambavyo havina alama halali za utambulisho.'

UHAKIKI WA VYETI:
Waziri Angela Kairuki asema vyeti 1,538 vinatumiwa na watumishi wa umma 3,076, ambapo cheti kimoja kinatumiwa na mtumishi zaidi ya mmoja.11,596 waliwasilisha vyeti pungufu.'

SHAMBULIZI KWA WAANDISHI:
Prof Lipumba alitaka Jukwaa la Wahariri kuchukua hatua za kisheria dhidi ya walioshambulia waandishi wa habari katika mkutano wa CUF.'

UHAKIKI WA VYETI:
Rais Magufuli aagiza watumishi wa umma 9,932 waliogushi vyeti wafutwe kazi, na watakaosalia hadi tarehe 15 Mei wafikishwe mahakamani.'

VURUGU CUF:
Watu 7 wakiwemo Mkurugenzi wa habari CUF Abdul Kambaya wakamatwa na polisi wakihusishwa na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa CUF hivi karibuni.'

UHAKIKI WA MIKOPO:
Naibu Spika Dk Tulia Ackson, mjini Dodoma, awaambia wabunge waliosoma kwa mkopo kujaza fomu za uhakiki ili kuepuka kushtajiwa kortini.'


UBUNGE EALA:
Uchaguzi wa nafasi 2 za wabunge wa Bunge la Africa Mashariki(EALA) kupitia Chadema kufanyika Mei 10, Katibu wa Bunge Thomas Kashililah atangaza leo.'


BREAKING NEWS ZA TAREHE 27/04/2017
MATOKEO LA LIGA:
Barcelona yaifunga Osasuna mabao 7-1, Lionel Messi, Andre Gomes na Paco Alcacer wakifunga magoli mawili kila mmoja.'

UDHALILISHAJI MIGODINI:
N/Waziri wa kazi A.Mavunde asema serikali itawachukulia hatua waajiri migodini wanaodhalilisha wafanyakazi kwa kuwapekua sehemu za siri.'

AJALI PWANI:
Mtu mmoja ahofiwa kufa na wengine 27 wanusulika baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama bahari ya Hindi wilayani Rufiji, Polisi yathibitisha.'

KESI YA UCHAGUZI:
Korti Kuu Arusha yatoa siku 14 kwa aliyekuwa mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole kuandika notisi ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliomtengua ubunge.'

AKIBA YA CHAKULA:
Akiba katika ghala za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula yapungua kutoka tani 86,834 January hadi tani 86,444 February 2017, BOT yaeleza.

WATUMISHI WAADHIBIWA:
Baraza la madiwani Geita lawafukuza kazi watumishi wawili wa halmashauri kwa utoro kazini an kuwasimamisha wengine wawili kupisha uchunguzi.'

UCHAGUZI KENYA:
Muungano wa vyama vya upinzani huko Kenya National Super Alliance (NASA)wampitisha waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga kugombea kiti cha urais.'

UHAKIKI VYETI:
Waziri Angellah Kairuki kumkabidhi Rais Magufuli ripoti ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika ukumbi wa Chimwaga, Dodoma, Ikulu yasema.'

TUHUMA IRINGA:
Polisi inamshikilia aliyekuwa M/kiti wa CCM Iringa, Jesca Msambatavangu kwa tuhuma za kuratibu mauaji ya mwanamke mmoja, RPC Mjengi athibitisha.'

TUHUMA-USAHIHI:
Mwanamke anayedaiwa kushambuliwa na aliyekuwa M/kiti wa CCM Iringa Jesca Msambatavangu hakufariki-kamatulivyoripoti bali alipata maumivu makali.'

0 Maoni :

Post a Comment