OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

Jinsi ya kuunganisha Kompyuta Mbili ziweze kuwasiliana (Kutumiana File/Folder na hata kucheza Game)

Kwanza yapaswa ufahamu kuwa ili kitu chochote kiweze kuwasiliana na kingine yahitaji kila kimoja kiwe na kitambulisho pekee kinachomwakilisha, nina maana kwamba Kwa mfano ili uweze kuongea na rafiki yako kama yupo mbali mtahitaji kila mmoja wenu awe na namba ya simu, namba ya simu humtambulisha mtu pekee katika kampuni fulani mfano Vodacom(0754,0763...),Kwa mazingira hayo ili Kompyuta nayo iweze kuunganisha na kompyuta nyingine huwa inahitaji IP Address na kila IP address huwa zinakuwa kwenye Class tofauti MfanO Class A(10.0.0.0).

Hivyo basi hatua ya kwanza ya kufanya hakikisha kila kompyuta imepewa IP address ya Class yeyote utakayopendekeza Mfano (192.168.100.2) Hii ni IP address ya Class C.

Fahamu kuwa IP address hazitakiwi kufanana na hakikisha kama unatumia Class C basi Kompyuta zote weka class C, Mfano Kompyuta ya kwanza naweza weka 192.168.137.1 na ya pili naweka 192.168.137.2

HATUA ZA KUWEKA IP ADDRESS KWENYE KOMPYUTA

1. Ingia Control panel

2. Bonyeza View Network status and tasks

3. Bonyeza Change Adapter Settings

4. Right Click Local Area Connection, kisha Bonyeza Properties

5. Chagua internet protocal version 4 (TCP/IPv4), Kisha Bonyeza Properties

6. Chagua Use the following IP address, Kisha Andika IP address utakayopendekeza kama nilivyokuonesha kwenye mfano wa Class C.

7. Bonyeza sehemu ya kuweka address kwenye Subnet mask, hapo itaandika yenyewe baada ya kuandika IP address yako kwani huwa inatambua Class ya Address uliyoandika juu.

8. Bonyeza OK

9. Bonyeza Close.

Hapo utakuwa umemaliza,

FANYA HIVYO PIA KWENYE KOMPYUTA YA PILI na kuipa IP address yake.

Baada ya kukamilisha zoezi la kuzipa IP address Sasa unatakiwa kuruhusu kompyuta zako ili ziweze kufanya Sharing


JINSI YA KURUHUSU SHARING SETTING

1. Ingia Control panel

2. Bonyeza View Network status and tasks

3. Bonyeza Change Advanced Sharing Setting

4. Ruhusu kwa kubonyeza Turn on Network discovery, Sharing na zinginezo ila kwenye Sehemu ya password unapo turn off, tambua Mtumiaji wa kompyuta ya pili ataweza ku share mafile yako bila kudaiwa password ya kompyuta yako. ni vema uka turn on.

Mpaka hapo utakuwa umemaliza.


Sasa Unganisha LAN Cable ya RJ45 Kwenye port zake kwa Kompute Moja hadi Nyingine kama ilivyonesha kwenye picha hapo chini





Ili kuona Files au Folder Kwenye kompyuta ya nyingine:

1. Ingia Control panel

2. Bonyeza View Network status and tasks

3. Bonyeza Multiple Networks, Hapo utaikuta Jina la Kompyuta unayo share.

Ingia kwenye kompyuta hiyo kisha Unaweza Kutumia mafile yake yote kwenye folder la USER


*Asante kwa kuendelea kutembelea ICT yetu...............Andika Maoni yako yeyote hapo chini..*


TAZAMA VIDEO FUPI HAPO CHINI KAMA HUJAELEWA MAELEZO YANGU HAPO JUU


Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Maoni :

Post a Comment