OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

Ufanye nini endapo Kompyuta yako haiwaki kabisa?

Wakati mwingine Kompyuta zetu huwa zinawaka lakini hakuna kitu kinachoonekana kwenye kioo, Hupati kiashiria chochote kuwa imewaka kioo ni nyeusi tu. au huweza ona taarifa kwenye kioo kuwa "No VGA cable" au "Check the Video cable" error. Kwa tatizo hilo kuna vitu vingi huweza kusababisha, Na ili iweze kuwaka kama kawaida itabidi utatue/urekebishe baadhi ya vitu katika kompyuta yako,

Twende pamoja kwa hilo somo ili kutatua tatizo lako, ili kompyuta yako irudi katika hali ya kawaida




Sawa hapo Swali ni kipi kulichosababisha mpaka Kompyuta yako isiwake? na jinsi gani ya kuweza kutatua hilo tatizo? Jibu litapatikana ni baada ya kufanya hatua zifuatazo moja baada ya nyuingine:



HATUA YA KWANZA:

Angalia kioo (Monita) yako Vizuri; Kitu cha kwanza inabidi ujidhihirishe kuwa je Monita yako inapata umeme na inawaka? Siyo hivyo tu bali je waya wa data (VGA cable) imechomekwa vizuri? Huwaenda pini zake zimekatika au kupinda.



HATUA YA PILI:

Angalia kadi ya picha (Graphic Video Card); Fungua ndani ya kompyuta yako na uhakikishe kadi ya picha imechomekwa vizuri kwenye saketi (Motherboard). Jaribu kuitoa hiyo kadi Safisha vumbi alafu irudishie tena kwa kuiweka sahihi, na uwashe tena kompyuta yako, ili kujua kuwa huenda tatizo likawa hilo. Kama kompyuta yako imewaka basi ulikuwa na tatizo la Kadi ya picha.


HATUA YA TATU:

Angalia Vifaa vingine ndani ya kompyuta: Wakati mwingine baadhi ya vifaa (Hardware) kama havijachomekwa vizuri kama HDD,CD ROM yaweza sababisha tatizo hilo, hakikisha unachomoa vyote na kuchomeka tena upya, kisha washa tena kompyuta yako.

HATUA YA NNE:

Angalia CMOS Battery; Wakati mwingine CMOS battery linapochoka au kukaa vibaya huwa linasababisha tatizo lingine kama la kutokuwa kompyuta na hata lingine zaidi, hivyo basi jaribu kulitoa pia na uliweke tena vizuri na uwashe tena kompyuta yako, kama tatizo siyo hilo tuendele na hatua nyingine




HATUA YA TANO:

Angalia RAM; Kuna asilimi 90 ya tatizo la RAM husababisha kompyuta kuto kuwaka, kwakuwa hapo ndipo sehemu muhimu sana ni kama njia ya kutoka kwenye ubongo na kutuma taarifa sehemu zingine. Endapo kama RAM imekufa Kompyuta haiwezi kutoa picha kwenye kioo (Monita) na hata sakiti (Motherboard) wakati mwingine haitowaka. Sasa kama una RAM mbili kwenye kompyuta yako jaribu kutoa moja na uache moja kisha washa kompyuta yako, kama bado jaribu uliyotoa au weka kwenye shimo (slot) nyingine huenda RAM moja au Shimo (slot) moja imekufa. Pia hakikisha unapotoa hizo RAM una zisafisha vizuri makalio yake, kama hujui jinsi ya kusafisha tafadhari andika Comment mwisho wa post hii ili nikuelekeze, maana hapo unahitaji kuhakikisha kuwa kila kitu kipo sawa ndipo twende hatua inayofuata.






HATUA YA SITA:

Angalia Ubongo wa Kompyuta (CPU); Hii ni hatua ya mwisho baada ya kushindikana kwa vyote, kwa kuwa ubongo wa kompyuta ni mara chache sana kuharibika, ni kama asilimia 1 tu ya tatizo la ubongo (CPU), Jaribu kutoa ubongo Safisha vizuri na uweke tena, huenda labda umekaa vibaya. Kisha washa tena kompyuta yako.



Kama hujaweza kufanikiwa kwa hizo hatua zote Comment au tuma email; ajakai17@gmail.com ili niweze kukusaidia zaidi. Asante
Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

11 Maoni :

  1. Nina tatzo naitaj tuongee moja kwa moja kuhusu lap top yang aina ya dell

    ReplyDelete
  2. Pc imezima gafla iliwekwa kwenye charge kuanzia usiku hadi asubuhi na angalia haiwaki

    ReplyDelete
  3. mimi kompyuta yangu aina ya hp yenyew inawak then ile fan au aic inazunguka kwa speed na kupiga kelele lakin kwen monitor hkuna kinachowaka an inaandika no input signal

    ReplyDelete
  4. ☝🏽 please help me 0624480068

    ReplyDelete
  5. Kompyuta yangu INA fika mpaka kwenye f1 halafu inajizima samtime INA Sasha tu fen kwa nguvu afu haioneshi kitu kwenye kioo

    ReplyDelete
  6. prease help me 0788182858 desktop yangu haiwaki

    ReplyDelete
  7. Nina laptop yangu kampuni ya compac kila nikiwasha taa zinawaka kuonuesha imewaka lakini kioo hakionyeshi kitu na sehemu za kuchomeka mouse nikichomeka hazionyeshi kuwaka keyboard haifanyi kazi shida itakuwa shida nini nduguyangu

    ReplyDelete
  8. Hi I really appreciate it worked out

    ReplyDelete
  9. Mimi laptop yangu natumia ramu 6GB ambayo ni 4gb na 2gb sasa niliitoa 2gb nikaweka 4gb ili ziwe 8gb inawaka inazima na hiyo ramu ni nizima nikiiweka kwenye laptop nyingine inawasha shida nini

    ReplyDelete