OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

Je, unahitaji kuunganisha TV (LCD, LED,Plasma) na Laptop yako? Ni rahisi sana, Fanya hivi:

Huenda Laptop yako ina kioo kidogo au unapenda kutumia Flat screen TV yako kama monitor au display ya laptop yako, basi Pitia hatua Nne tu ili kuunganisha TV na Laptop yako.



Hatua ya Kwanza: Utambue Port za TV yako

a) Unahitaji VGA Cable au HDMI cable kuunganisha Laptop kwenda LED/LCD/Plasm Tv’s.

b) Angalia Connections zilizopo kote kwenye TV na Laptop

c) Hapo chini kuna orodhaa kadhaa za ports zilizopo maarufu kwenye LED/LCD/Plasma TV’s



Hatua ya Pili: Utambuzi wa cables

a) Hapo chini kuna orodhaa kadhaa za cables zilizopo maarufu


b) VGA cable ita sapport kwenye display ya laptop tu kuunganishwa na TV. Kwa ku share sauti pia unahitajika kupata AUX in cable.

c) HDMI cable inapendekezwa sana kama ku transmit vyote signal za sauti na video kwenda kwenye TV

Hatua ya Tatu: Kuunganisha TV


a) Zima TV na Laptop

b) Unganisha HDMI au VGA cable kwenye slot zake husika kwenye TV ambazo huwa zinapatikana nyuma / pembeni(ubavuni) mwa TV

c) Unapomaliza kuunganisha washa kwanza TV na kufuatiwa na Laptop

Hatua ya Nne: Settings za Laptop

a) Bonyeza kitufe kilichoandikwa “Source” kwenye Remote ya TV na chagua HDMI kama HDMI cable imeunganishwa au PC kama VGA imeunganishwa

b) Kwa jinsi ilivyo, unapounganisha TV kwenda PC, taswila/ image ile ile ya desktop itaonekana kwenye TV c) Locate extend ya Video function key kwenye keyboard (itakuwa tofauti kwa laptop zote) na bonyeza hiyo wakati umebonyeza function (Fn) key kwenye keyboard

d) Hapo chini kuna orodhaa zilizopo za uchaguzi /option

1. Laptop Only

2. External Display Only

3. Clone Display ( Laptop + External Dispaly)

4. Extend Display ( Display will be extended to the TV)

e) Chagua Output unayoitaka kuitumia

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI KAMA HUJAELEWA
Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Maoni :

Post a Comment