Lakini hebu tazama tena mwonekano wake baada ya kubadili Theme ya screen
Home screen |
Application Screen |
Kwakweli inavutia hata kama nikipiga snapshot mtu kwa haraka haraka ni ngumu sana kugundua kuwa hii ni Tecno Y4
Siyo Icon tu, bali pia unaweza kubadili style ya maandishi ya simu yako(Font style).
Ili kubadili mwonekano wa simu yako huenda umechoka na mwonekano wake, tafadhari fuata hatua zifuatazo:
JINSI YA KUBADILI MWONEKANO WA ICON ZA SIMU/THEME
>>Ingia kwenye playstore ya simu yako
>>Andika Theme for Android kwenye sehemu ya Search(zitakuja Theme nyingi sana)
>>Chagua Theme unayoipenda katika mwonekano (Shusha mpaka chini ili kutazama itakavyoonekana baada ku install kwenye simu yako)
>>Bonyeza Install
Baada ya kumaliza installation, Fungua (Theme hizo mara nyingi huwa zinategemea App nyingine ili kufunguka), Sasa basi unapoifungua itakuamuru kupakua tena App nyingine ambayo itakupeleka moja kwa moja bila kutafuta, cha msingi wewe ni kuikubalia tu ili uweze kuipakua na hiyo App.
Baada ya kumaliza ku install App hiyo ya mwisho(third part), utachagua Theme au uta acha ile ya default kisha SET theme. Hapa utakuwa umemaliza na mwonekano wa simu yako utakuwa tayari umebadilika baada ya kufuata hatua zote zilizo kuamuru.
JINSI YA KUBADILI MWONEKANO WA MAANDISHI KWENYE SIMU YAKO(FONT SYLE)
>>Ingia kwenye playstore ya simu yako
>> Andika iFont kwenye sehemu ya Search au bonyeza >>iFont
>> Ipakue na install kwenye simu yako
>>Chagua aina ya maandishi unayopenda(utakachochagua, utabonyeza download kisha SET)
Unapobonyeza SET itakuamulu ijizime simu na kujiwasha ili ihifadhi mabadiliko
Baada ya kuiruhusu kujizima, itakapowaka itakuwa tayari imebadili mwonekano wa maandishi.
Mpaka kufikia hapo tumefikia mwisho wa somo letu. Tafadhari usisahau kuuliza swali lolote au Comment chochote kama ushauri kwenye page zetu. ICT yetu ni yetu sote kwa kupambana na matatizo mbali mbali ya kompyuta na ICT Kwa ujumla………Asante!!!
Good
ReplyDelete