OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

Mbunifu wa Android azindua simu mpya ya Essential

Bwana Rubin aliacha kazi katika Google mwaka 2014 kwa ajili ya kubuni kampuni yake ya uwekezaji wa kiteknolojia.


Essential ni moja wapo ya kampuni zinazodhaminiwa na kampuni ya Rubin - na simu ya Essential ni moja bidhaa zake.
  • Simu ambazo hazifanyi kazi tena na WhatsApp
  • Simu ya Samsung yashika moto kwenye ndege
  • Simu ya Samsung yashika moto kwenye ndege

Simu hiyo hutumia mfumo wa Android na imeanza kuuzwa nchini Marekani kwa dola $699.

Hata hivyo, itakuwa ni vigumu kwa kampuni hiyo kujipenyeza katika masoko makubwa ya ambayo tayari yameimarisha mauzo ya bidhaa zake nchini humo.

Samsung kwa sasa ndio yenye soko kubwa la hisa katika soko la simu za Smart, ikiwa na mauzo ya asilimia 21% kote duniani, kulingana na mchambuzi wa masuala ya makampuni Gartner. Apple ina soko la asilimia 14%.


Licha ya makampuni makubwa ya Uchina yanayouza simu zenye gharama ya chini, viwanda vidogo vidogo vimepata ugumu wa kupata walau asilimia moja ya hisa kwenye soko za bidhaa zao - na bei ya simu ya Essential inaiweka kwenye hali ya changamoto kubwa zaidi

Lakini Bwana Rubin aliiambia hadhira ya watu mjini California kwamba anaamini kuna nafasi ya soko la Android kwa muuzaji mwingine licha ya Samsung, na kwamba Essential inalenga kuwa kampuni kuu inayotoa aina mbali mbali za bidhaa kwa mnunuzi

Essential phone imetengenezwa kwa madini ya titanium na ina kioo kilichoenea sehemu kubwa ya simu na sehemu isiyo na kioo ni ndogo zaidi.



Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Maoni :

Post a Comment