Kazi za msingi za kompyuta
Kazi za uingizaji (Input).
Kazi za uwendeshaji au ufanyishaji (Proccessing).
Kazi za utoaji (Output).
Kazi za kuhifadhi (Storege)
Matumizi ya kompyuta
Elimu:
Kutokana
na kuendelea kwa elimu ya teknolojia imetusaidia sana kujifunza mambo
mbali mbali kupitia kompyuta, ambapo unaweza kutumia kompyuta kwa ajili
ya kuuliza maswali na kujibiwa kwa haraka tena kwa njia tofauti, pia
unaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kielimu,
pia unaweza kuandaa vipindi mbali mbali vya masomo na kufundishia elimu
tofauti. Pia unaweza kuonyeshea filamu zenye mafundisho mazuri, kama
kuonyesha filamu zenye elimu ya jeografia na sayansi ya mifugo na
kilimo, kuonyesha sehemu muhimu za nchi yetu, kuonyesha athari za nchi
ambazo ndiyo sehemu kuu zinazotuletea fedha za kigeni katika nchi yetu,
na kuonyesha picha za maendeleo katika sekta mbali mbali za nchi yetu,
pia kuonyeshea mila na tamaduni za taifa letu la Tanzania na mataifa
mengine mbali mbali duniani n.k.
Michezo:
Kompyuta zimeandaliwa ndani yake programu mbali mbali
zenye michezo tofauti, ambayo inaweza kutumika na watu mbali mbali
kutofautiana na umri wao, na ambayo inajulikana kama moja ya kazi za
kukuza kipaji na kuchangamsha akili, na ni sehemu moja wapo ya
kuburudisha nafsi.
Ufundi:
Kompyuta zinaweza kutumika kwa
ajili ya kufanyia kazi za ufundi, kama kuchora ramani ya nyumba na
mazingira ya nje ya nyumba, kutengenezea picha kwa kuibadilisha na
kuiremba na kuifanya ionekane katika sura nyengine ambayo tofauti na ile
ya asili.
Mawasiliano:
Kompyuta inaweza kutumika kwa
ajili ya kufanyia mawasiliano kupitia mtandao wa (Internet) ambao leo
hii ndiyo umeshika nafasi kubwa sana ya mawasiliano kuliko kitu chengine
ulimwenguni, kama kuwasiliana kwa kutumiana ujumbe wa barua pepe
(E-mail) ambayo ni rahisi na inafika haraka kuliko barua za kupitia
posta, pia kwa kutumia barua pepe hakuna haja ya kufikiria sehemu aliko
mtu America au Asia au sehemu nyengine duniani, kuwasiliana kwa maneno
ya maandishi (Chat), pia kuwasiliana kwa maneno ya sauti na kuonekana
picha.
Usafirishaji:
Kwa kutumia kompyuta unaweza
kuendeshea kazi za usafirishaji katika vituo vikuu vya usafirishaji,
kama usafiri wa ardhini (mabasi, metro na treni), usafiri wa majini
(meli), na usafiri wa angani (ndege).
Matumizi ya kiwandani:
Kama
kuendeshea mashine viwandani kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbali mbali,
kama kutengenezea magari, kuzalishia umeme na kutengenezea bidhaa
nyengine za kawaida kama nguo mazulia n.k.
Matumizi ya benki:
Kama
ilivyokuwa ada na kawaida hivi sasa kutumia kompyuta kwa ajili ya
kuendeshea kazi za benki,kwa ajili kurahisisha kazi za mahesabu.
Kufanyia matibabu:
Kompyuta
zimekuwa na matumizi makubwa na muhimu sana katika kufanyia uchunguzi
na matibabu hospitalini, kama kuchunguza na kuelekeza dawa ya kutibu
ugonjwa uliyoonekana, pia kupimia na kujaribia mimba na kutoa maelekezo
kuhusiana na siku na tarehe ya kujifungua.
Kazi za kompyuta
1. Kuhifadhi vitu (Data):
Kama
ilivyotanguliwa kusemwa hapo awali kuwa kompyuta ni chombo pekee chenye
uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu, na mpaka hivi sasa bado hakijapatikana
chombo chengine chenye uwezo mkubwa wa kuhifadhia vitu zaidi ya
kompyuta.
2. kuonyeshea matokeo ya vitu (Data na Information):
Kutokana
na kuendelea elimu ya teknolojia imeweza kuturahisishia kazi zetu
nyingi ambazo tulikuwa tunazifanya kupitia vyombo mbali mbali, na kila
chombo kilikuwa na kazi yake maalumu, tofauti na kompyuta ambapo mtu
anaweza kuanzisha au kutengeneza kitu na wakati huo huo anaweza
kukionyesha kwa kutumia kompyuta yenyewe, yaani kuonyesha ufanisi na
sura nzuri ya kitu kilichofanyika.
Sehemu kuu mbili za kompyuta
1.
Sehemu zinazoshikika (Hardware) Sehemu zinazoshikika (Hardware), ni
aina zote za vifaa vya kompyuta, navyo vimegawanyika katika sehemu kuu
tatu.
Vifaa vya kuingizia vitu (Input devices):
kibodi (keyboard)
Mausi (Mouse)
Skana (Scanner)
Makrofoni (Microphone)
Kamera (Camera)
1. KIBODI (KEYBOARD):
Kibodi
inatumika kwa ajili ya kuingizia herufi, namba, alama na michoro, nayo
imegawanyika katika sehemu kuu nne, nazo ni kama ifuatavyo: Funguo za
kuandikia (Typewriter keys), funguo za kuhama (Movement keys), funguo za
namba pamoja na michoro mingine (Numeric keys) na funguo za kazi
Function keys).
elewa maana ya vitufe vya kibodi ya kompyuta
Home natumika kwa ajili ya kuhamia mwanzo wa mstari
End Inatumika kwa ajili ya kuhamia mwisho wa mstari.
Pg Up Inatumika kwa ajili ya kuhamia juu ya mstari.
Pg
Dn Inatumika kwa ajili ya kuhamia chini ya mstari. Num lock Inatumika
kwa ajili ya kufunga na kufungulia namba na michoro. Caps lock Inatumika
kwa ajili ya kufunga na kufungulia. Enter Inatumika kwa ajili ya
kutekeleza amri, au kuanzisha fungu la maneno kwenye ukurasa.. Del
“Delete” Inatumika kwa ajili ya kufuta herufi ya mbele yake. “Back
space" Inatumika kwa ajili ya kufuta herufi ya nyuma yake. Space “Space
bar” Inatumika kwa ajili ya kuweka masafa kati ya maneno. Esc “Escape”
Inatumika kwa ajili ya kuacha kutekeleza amri. Tab Inatumika kwa ajili
ya kuwacha masafa maalumu tofauti na ya kawaida (Normal).
0 Maoni :
Post a Comment