Rufus ni programu inayokuwezesha kufanya bootable USB flash yako kwa ma file ya .iso, Programu hii ni rahisi sana kutumia na wala huchukui muda mrefu kufanya bootable flash, ni tofauti kidogo na Power iso au zinginezo.
Kabla ya kupakuwa programu hiyo Soma maelezo kidogo ya jinsi ya kutumia:
1. Pakua programu ya Rufus kwa kubonyeza kitufe cha Pakua programu hapo chini (Ukipakua wala huitaji istallation ni kufungua tu na kuanza kutumia)
Na hakikisha unafahamu file lako la .iso lilipo kwenye kompyuta yako
2. Ingiza Flash yako unayotaka kufanyia bootable, hakikisha ukubwa wa flash inaweza kuingiza file lako .iso
2. Fungua Programu yako ya Rufus
3. Bonyeza sehemu ya browse (kwenye icon ya CD) ili uchukue file lako la .iso kwenye kompyuta yako
Kisha bonyeza Start
Subiri kwa muda mpaka itakapomaliza ku Upload ma file kwenye flash, Baada ya kumaliza Bonyeza Close. Utakuwa umemaliza.
Sasa unaweza kutumia flash yako. Kama umehifadhi Window basi ingiza kwenye PC yako unayohitaji kupiga window kisha chagua USB FDD kama First priority kwenye BIOS, Kisha zima na kuwasha kompyuta yako. Automatic ita boot kwenye flash na kuendelea na hatua za kuweka window.
Home
/
pakua
/
Fanya Bootable flash ili uweke window kwenye PC yako kwa kupakua Programu ya Rufus BURE (Easy to use)
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 Maoni :
Post a Comment