Matangazo huwa yanaboa sana pale unapofungua App yako uliyo pakua au unapotaka kucheza Game. Kuna form nyingi za matangazo huwa zinajitokeza tokeza ovyo kama vile muundo wa banner na hayapotei mpaka uyafunge na huenda likatokeza lingine, matangazo ya Flash huwa yanachukua screen nzima na Popup angalau huwa yanawekwa kwa muda, baada ya muda fulani huwa yanapotea yenyewe. Kwa upande wao wenye hayo matangazo huwa yanafaida kwako kwani huwa wanaingiza kiasi cha pesa kila mwezi, na mengine yanakulazimisha ulipie gharama fulani baada ya kukubali. Sasa kuanzia leo utakuwa umeachana na usumbufu huo na utapakua App nyingi bila kupata matangazo yeyote baada ya kufuata hatua zifuatazo kwenye simu au kifaa chako Kuna App ambayo ni nzuri sana kuitumia kwa kuzuia matangazo hayo, inajulikana kama AdAway; Kwanza tuanze kuifahamu kidogo
AdAway ni nini?
AdAway ni App/programu imayofanya kazi ya kuzuia/kufunga matangazo pale unapoperuzi kwenye internet. itazuia matangazo kwa kuboresha HOSTS file ya smartphone au tablet. inaweza kuzuia matangazo kutoka kwenye browser zote,apps, games, websites na zinginezo. ili iweze kufanya kazi inahitaji kifaa chako kiwe na access ya Root, inamaana AdAway inapatikana kwa simu zote zilizokuwa rooted. Kama Simu yako haijawa rooted basi pia ondoa shaka, KingoRoot ni moja ya programu inayotumika ku root simu yako, Tafadhari bonyeza >> KingoRoot ili kuroot au kama kifaa chako tayari kimeshakuwa rooted basi tuendelee na hatua zinazofuata.
Jinsi ya kupakua AdAway
App hiyo haipo kwenye Google Play, hivyo basi unahitajika kupakuwa kutoka kwenye mitandao, au tafuta kwenye google kwa kuandika "download AdAway" au bonyeza AdAway kupakua.
Jinsi ya kutumia AdAway kufunga matangazo
Unapofungua App yako kwa mara ya kwanza itakuuliza kama umesha root simu/kifaa chako, bonyeza OK kupata access
Bonyeza"Download files na apply ad blocking" button app itapakua na ku apply hosts file kisha itaanza kuzuia matangazo.
Inapomaliza na kukamilisha utapata pop up ku reboot simu yako. siyo lazima ku reboot unaweza uka reboot au la.
Unaweza uka scan matangazo kwa Adware kutoka kwenye menu.
Simu yako ya Android smartphone au tablet inapomaliza hatua hizo na kukamilisha, matangazo yote yatakuwa yamefungwa. AdAway inafaida kwamba huitaji tena kuzuia matangazo labda utakapo update simu yako, kwani huitaji tena kufanya hatua hizo. wewe ni kupakua tu Apps au games zozote bila kupata matangazo tena.
Tazama video hapo chini jinsi ya kuzuia matangazo kwa kutumia AdFree
Tazama video hapo chini jinsi ya ku root Simu yako kwa kutumia Kingo Root
0 Maoni :
Post a Comment