OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

Jinsi ya kujitengenezea Network/Mtandao nyumbani au Sehemu ya Biashara(mfano: Internet Cafe)

Kama unahitaji ku share mafile au internet kutoka Kompyuta moja hadi nyingine au kutoka Kompyuta moja hadi kifaa kingine kilichounganishwa kwenye mtandao huo mmoja mfano printer. Basi yapaswa kuunganisha kompyuta hizo pamoja na vitu vingine unavyotaka viwasiliane. Unaweza kufany ahivyo kwa kompyuta zako zilizopo nyumbani au hata sehemu ya biashara kama internet Cafe. Fuata hatua zifuatazo ili kukamilisha zoezi hili:

VITU VYA KUANDAA

1. Kompyuta zaidi ya mbili unazotaka kuunganisha kwenye Network

2. Waya za ethernet Cable, UTP cable urefu usizidi m 100

3. Printer (kama unayo, na kama huna achana nayo)

4. Switch ya port 4 au 8 na kuendelea, hii inategemea na idadi ya kompyuta ulizonazo

5. Modem au Router kama unahitaji kutumia na Internet



JINSI YA KUUNGANISHA

1. Tumia UTP cable kwa kila Kompyuta, yaani chomeka kutoka kwenye port yake RJ 45, Mpaka kwenye port ya Switch kwa kila kompyuta.

2. Unaweza ukatumia Trunk ili kuficha waya za UTP zisionekane kama uchafu, yaani kwa kugongea ukutani kutoka kwenye switch sehemu iliyopo mpaka kwenye Kompyuta husika kama ulivyoonesha mchoro hapo chini

3. Baada ya kuona kuwa kila kompyuta inasoma kwenye Switch yaani angalia idadi ya kompyuta ulizounganisha kwenye switch na idadi ya taa zinazowaka kwenye switch.
Baada ya kujihakikishia hayo, Basi Soma hatua ya kuzipa IP address Kompyuta zako ili ziweze kukutana kwa kubonyeza HAPA>>

 Baada ya kumaliza zoezi la kuzipa IP address Kompyuta yako na kufungua au kuruhusu sharing files, utakuwa umefanikiwa kutengeneza network yako. Ila kama unahitaji kutumia Internet Basi Bonyeza HAPA>> ili kuhua jinsi ya kuunganisha Modem au Router kwenye Network yako ili upata Internet kwa kompyuta zote ulizonazo.


TAZAMA HAPA UFAHAMU JINSI YA KUTENGENEZA UPT CABLE ZAKO




  TAZAMA VIDEO HII KUJIFUNZA ZAIDI JUU LA SOMO LETU LA LEO




Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Maoni :

Post a Comment