Leo March 8 2017 ni siku ya Wanawake Duniani hivyo sio vibaya kama tukicheki michango mbalimbali iliyofanywa na wanawake katika sekta muhimu ya sayansi na teknolojia ambapo mara nyingi hutawaliwa na wanaume. Nimekuletea list ya wanawake kumi waliyofanya uvumbuzi wa vitu mbalimbali ambavyo vilibadilisha historia ya teknolojia duniani.
1:Florence Parpart. Mwaka 1914 Florence Parpart alivumbua friji la kisasa linalotumia umeme ambapo uvumbuzi huo uliweka rekodi ya dunia hasa baada ya kuvumbuliwa na mwanamke.

2: Marie Van Brittan. Anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa katika uvumbuzi wa kamera za CCTV mwaka 1969, ambapo ugunduzi huu aliufanya baada ya kukithiri kwa uhalifu katika jiji la Newyork.

3: Stephanie Kwolek atakumbukwa kwa uvumbuzi wake wa material yaliyotumika kutengeneza bullet proof, vikoti ambavyo huvaliwa kwa ajili ya kuzuia risasi isiingie mwilini.

4: Hedy Lamarr: Ni mwafizikia aliyebobea katika maswala ya mawasiliano ambapo aligundua teknolojia ya wireless iliyosaidia kuanzishwa kwa wiFi na mfumo wa GPS.

5: Josephene Cochrane. Mwaka 1887 Josephene Cochrane alivumbua machine ya kuoshea vyombo au dish washer ambazo alikuwa akiziuza mahotelini mwaka mmoja baadae alifungua kiwanda chake.

0 Maoni :
Post a Comment