OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

'Madhara ya Minara ya Simu kwa binadamu' na Tamko kutoka TCRA kuhusu kauli hiyo

Teknolojia ya simu hutumia mionzi ya masafa marefu ambayo inajulikana kwa lugha ya kitaalamu kama“wireless microwave radation”, techinologia hii inaendelea kwa kadri siku zinavyozidi kwenda na watuwengi wanapendelea na kukimbilia kuishi sehemu zenye mtandao kwa sababu za urahisi wa kimawasiliano.

Mawasiliano hayo ya simu usafiri toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa njia ya minara ya simu. Sehemu yoyote ile ambayo unaoweza kupiga au kupokea simu tambua kunamtandao unaosambazwa na minara hiyo.
Sehemu ambazo minara ya simu imeonekana kuwa na mionzi mikali zaidi ni milimani na kwenye miinuko nje ya miji. Mionzi hii ina madhara kwa binadamu,mimea na viumbe hai vingine kama wanyama sababu hupata dozi ya moja kwa moja kutokana na kukosekana kwa vizuizi” obstruction/ barriers” hali inayofanya mionzi kusafiri moja kwa moja kutoka kwenye chanzo hadi kwa viumbe hai, na hii hupelekea kiwango cha dozi ya mionzi kuwa kikubwa kwa muda mrefu.

Mionzi hii inauwezo wa kusafiri katika umbali wa kuanzia mile 2 katika miinuko hadi miles 45 katika sehemu zenye vizuizi vichache(barrier) na ina uwezo wa wa kupenya hata kwenye ukuta na chuma. Minara hii inakuwa ni hatari zaidi endapo itatoa mionzi zaidi ya 1900 MHz. na hii imeonyesha kuwa na athari kwa viumbe hai wakiwemo banadamu wanaoishi ndani ya kilometa moja kutoka kwenye chanzo.

Pamoja na hayo ni vigumu kukimbia mionzi hiyo sababu ipo kila sehemu yenye mawasiliano japo nguvu ya dozi inapungua kulingana na umbali wa chanzo na watu,, kuwepo kwa vizuizi kama vile majengo ambayo yanauwezo wa kupunguza nguvu ya mionzi hiyo na kupunguza muda wa dozi husika.

Aidha tafiti mbalimbali za nchi zilizoendelea zimebainisha kuwa vuimbe hai vinavyoishi sehemu hizo vipo kwenye hatari zaidi ya kupata dozi kubwa ya mionzi hiyo. Mwili wa bianadamu wenyewe unauwezo wa kutoa dozi ya chini sana ya mionzi kama 10hertz, na kila chembechembe ya mwili wetu ina mionzi yake ( cellular electromagnetic field) ,Watafiti wamesema frequency za kutengenezwa zinazozidi 10 hertz zinaweza sababisha msongo wa mawazo, matatizo ya kukosa usingizi, matatizo ya kizazi na saratani mbailimbali endapo binadamu atapata dozi hiyo kwa muda mrefu.

Minara ya simu ina mionzi yenye nguvu zaidi kulinganisha na mionzi ya radio (the higher the frequency the more powerful the wave = more powerful effects on biological organisms) na kumbuka mionzi ya minara ya simu ina nguvu 1900 MHz. Mionzi hii inauwezo waa kuharibu bond ya molekula na chemicali na kusababisha mabadiliko ya vinasaba (DNA), Metabilism,vichocheo vya mwili (hormones) na enzyemes hali inayopelekea madhara yafuatayo ya kiafya:

1. Kuumwa kichwa(headache)
2. Kukosa kumbukumbu(memory loss)
3. Kupungua kwa mbegu za kiume za uzazi (low sperm count)
4. Saratani na kasoro za uzazi
5. Matatizo ya moyo
6. Msongo wa mawazo
7. Kukosa usingizi.

Kibaya zaidi mionzi hii ina tabia ya kujilimbikiza kwenye mwili (body accumulation) na kuja kuonesha madhara miaka kadhaa inayofuata kutegemea na mtu na mtu na hali ya afya ya mtu.



KUTOKA TCRA 

TCRA: Mionzi ya simu haina madhara

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA), imekanusha taarifa zinazodai mionzi inayotumika katika vyombo vya mawasiliano ikiwemo simu za mkononi, ina madhara kwa afya ya binadamu.


Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, aliyasema hayo Dar es Salaama March, 2013  katika warsha ambayo iliandaliwa kwa waandishi wa habari kuhusu mambo ya mionzi na matumizi yake katika jamii.

Alisema tafiti zilizofanywa nchini hivi karibuni, zimeonesha
hakuna madhara yeyote yanayosababishwa na mionzi ambayo inatokana na minara ya vyombo vya mawasiliano.

Aliviomba vyombo vya habari nchini, kutoa elimu kwa jamii ili kuwaondoa hofu wananchi waendelee kuvitumia vyombo hivyo zikiwemo simu za mkononi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu ya Atomic nchini (TAEC), Bw. Mwisarubi Nyaruba, alisema mionzi imegawanyika katika makundi mawili ambayo yametofautishwa kulingana na viwango vya kimataifa.

“Lipo kundi lenye kiwango kikubwa cha mionzi ambayo hutumika sana katika shughuli za hospitalini, kilimo, barabara na viwandani wakati kundi lingine lina kiwango kidogo na mionzi yake haina nguvu ambayo hutumika katika vyombo vya mawasiliano
zikiwemo simu za mkononi,” alisema.

Bw. Nyaruba aliongeza kuwa, vyombo vya mawasilano vinatumia kiwango kidogo cha mionziambayo haiwezi kuleta madhara kwa binadamu.

Wakati huo huo, Prof. Nkoma alisema TCRA haitasitisha mpango wa matumizi ya mfumo mpya wa digitali ambao umeanza rasmi Januari mosi mwaka 2013, katika baadhi ya mikoa nchini.

Juzi Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), waliiomba Serikali kuangalia namna ya kuurudisha mfumo wa analojia uende sambamba na digitali ili wananchi wapate muda
wa kujiandaa na mfumo mpya ambao umeonekana kuwaathiri
sana panmoja na vyombo vya utangazaji.
Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Maoni :

Post a Comment