Cha kusikitisha ni kuwa wapo wengi waliojiingiza kuitumia hiyo alama bila kujua maana yake na kazi yake, hivyo kumekuwa na utitiri wa hashtag zisizo na msingi wowote.
Katika makala hii utajifunza matumizi sahihi ya hashtag na wapi uitumie.
Kazi Ya Hashtag ni ipi ?
Katika mitandao ya kijamii ambapo hashtag hutumika , kazi yake ni kufanikisha ukusanyaji wa posts zenye ujumbe huo uliotajwa katika hashtag. Mfano kama umepost kwa Facebook na kuweka hashtag #memories, basi mtandao wa Facebook unaikusanya post yako na posts nyingine zote zenye kutumia hiyo hashtag ya #memories.
Kinachofuata baaadae, mtu yeyote akibofya hiyo hashtag yako ya #memories, ataletewa sio tuu post yako , bali ataletewa na posts nyingine za watu wengine waliotumia hiyo hashtag ya memories kutegemeana na namna gani watu hao waliruhusu posts zao ziwe kwa umma(public).
Wapi unaweza tumia Hashtag ?
Karibu mitandao yote mikubwa ya kijamii inatumia hiyo huduma ya Hashtag. Hapa ninamaanisha twitter, Facebook, Instagram, Google +, Pinterest, YouTube, Vine, na Flickr.
Matumizi ya Hashtag
1. Kurahisisha kupata taarifa
Hashtag hutumika na watu binafsi kukusanya posts zao sehemu moja, kwa maana ya kwamba mfano unataka picha zako za safari yako ya Mikumi National Park ziwe sehemu moja kwa urahisi siku ukitafuta, waweza tumia hashtag ya #safarimikumi kwa kila post utakayopost. Halafu siku ukitaka kuzipata posts zako, fanya kubofya hashtag husika , utaletewa posts zako nyingine. Angalizo kama umetumia hashtag ambayo ni rahisi watu wengine kuiandika basi jua unaweza letewa na posts za watu wengine waliowahi kuitumia. Hivyo kama unataka posts zako peke yako, jitahidi uwe na hashtag ya kipekee sana.
2.Hashtag inatumika kibiashara
Hashtag ikitumika na watu wengi sana, huitwa trending topic. Watu wengi hutafuta kujua hizo trending topic. Watu wa masoko hutumia ubunifu kuweza kutengeneza hashtag zenye kuwa trending topic, au hutumia hashtag ambazo tayari ni trending topic kuhusanisha matangazo yao na hizo hashtag. Hii inarahisisha watu kuona matangazo yao wakitafuta kujua kuhusu hizo hashtag.
Namna sahihi ya kutumia hashtag
Hakikisha hashtag neno unalolitumia kweli linaleta maana na linaendana na hicho unachokipost. Na hakikisha haujazi hashtag kibao katika post moja.
0 Maoni :
Post a Comment