OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

JINSI YA KUFUTA AKAUNTI YA FACEBOOK MOJA KWA MOJA (ISITUMIKE TENA)

Unatafuta mwongozo juu ya kufuta akaunti yako ya Facebook? Safi nitakuelekeza jinsi ya kufuta Akaunti yako ya Facebook Permanently.


Kuna sababu kubwa ya kwanini unataka kufuta Akaunti yako ya Facebook. Labda ni kuhusiana na Privacy au hata sababu zinginezo nyingi.

Kufuta au Kusitisha Akauti ya Facebook – Nini utofauti wa hayo?

Kuna njia mbili tofauti za kufanya Akaunti yako ya Facebook isipatikanike Mtandaoni/hewani. Ya kwani ni kusitisha, ambayo inamaana:
  • Unaweza ukairudisha tena Akaunti yako pale unapohitaji
  • Watu hawawezi kukuona kwenye Facebook Timeline, au wanapokutafuta sehemu ya Search
  • Baadhi ya Taarifa zitabaki zinaonekana kwa watu(kama meseji ulizotuma)
  • Facebook itatunza taarifa zako (kama marafiki na ulizovutiwa) ili uweze kuzipata pale unapoirudisha
Lakini Kufuta/Deleting Akaunti yako ni kitu ambacho unatakiwa kuwa makini sana. Kama utafuta Akaunti yako:
  • Facebook huwa inachelewa kufuta Akaunti hiyo baada ya siku chache mbele pale unapofuta. Kama utaingia Akaunti yako baada ya kufuta utakuwa umeirudisha tena/umezuia kufuta (subiri baada ya siku chache kupita ili Facebook waamini kuwa kweli unataka kufuta)
  • Hutakiwi kuingia tena kwenye Akaunti yako pale unapoifuta
  • Inaweza kuchukua mpaka siku 90 kwa kuondosha data zako ulizo hifadhi kwenye akaunti yako, ingawa kwa kipindi hicho taarifa zako huwezi kuzitumia
  • Kitu ambacho hukikihifadhi kwenye Akaunti yako, kama meseji ambazo hukuwahi kuzituma kwa marafiki – Hizo zitabaki kama Active/zinakuwepo
  • Copy ya material (kama log records) itabaki kwenye Database ya Facebook, lakini ni “disassociated from personal identiofiers,” kuhusiana na kampuni

Kawaida, kusitisha Akaunti ni njia bora zaidi kwenye Facebook, lakini kufuta tambua huondoka moja kwa moja ambayo haina njia, hivyo basi kuwa makini kabla hujaamua kufuta Akaunti yako

Jinsi ya Kusitisha/deactivate Akaunti ya Facebook

Fuata hatua zifuatazo ili kusitisha Akaunti yako:

1. Bonyeza Menu ya Facebook (kamshale kanapokaa juu kabisa ya browser yako upande wa kulia)

2. Chagua ‘Settings’

3. Chagua ‘Security’ kwenye colomn ya upande wa kushoto

4. Chagua ’Deactivate your account’. Na kisha fuata hatua ili kumalizia maamuzi yako

Kuirudisha tena baada ya kuisitisha, Ingia Facebook kisha ingiza Email au Namba zako za simu pamoja na Password/neon la siri, hapo itarudi tena.

Jinsi ya kufuta Akaunt ya Facebook

Bonyeza Link ya hapo chini ili ikupeleke haraka sehemu ya kufuta Akaunti yako:
Kabla hujafuta Akaunti yako, ni vema kupakua maelezo/habari zako kutoka Facebook. Ili kupakua/download habari zako fuata hatua hizi:

1. Bonyeza Menu ya Facebook (kamshale kanapokaa juu kabisa ya browser yako upande wa kulia)

2. Bonyeza ‘Download a copy of your Facebook data’ kwenye kitufe cha General Account Settings

3. Chagua ‘Start My Archive’
Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

3 Maoni :