OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

JINSI YA KULAZIMISHA SMARTPHONE YAKO KUTUMIA 2G, 3G AU 4G PEKEE

Kuna baadhi ya Simu huwa zina speed ya 2G ambayo ni kasi ya chini sana, na ungependa kuweka 3G, umejaribu njia nyingi hata kwa kuhamisha SIM Card lakini umeshindwa, Sasa unaweza uka command ili kuweka 3G au 4G kwa kufuata njia nilizokuwekea hapo chini. Kabla ya yote je, Unajua Internet?



Internet ni kitu cha muhimu sana na ambacho karibu watumiaji wote wa smartphones hukizingatia kwanza. Lakini kuna baadhi ya watumiaji wa smartphones wamekuwa wakikubwa na matatizo ya simu zao kutomuwa na mtandao wa internet ambao haueleweki mara 2g mara 3g, 4g pasipo ruhusa ya mtumiaji.

UNAJUA KWA NINI HALI HII HUTOKEA?
Frequencies za mtandao hubadilishana kutokana na matumizi ya internet kwenye eneo husika, hivyo suala la smartphone kujichagulia mtandao yenyewe hutegemeana frequencies za mtandao upi unaokuwa na nguvu ndani ya muda husika.

Kama frequencies za 2g, 3g au 4g Zitakuwa na nguvu basi smartphone yako itakachagua mtandao wa kutumia yenyewe.

KAMA SMARTPHONE YAKO INAJICHAGULIA 2G, 3G, AU 4G BILA WEWE KUPENDA BASI FANYA YAFUATAYO

Kwa Simu za Android

  •  NENDA SEHEMU YA KUANDIKIA NAMBA
  • BONYEZA >>> *#*#4636#*#* kama inakataa download application ya Phone testing
  •  Yatatokea machaguo kadhaa chagua #Phone information
  •  Shuka chini kabisa mpaka mpaka sehemu iliyoandikwa Set preferred network type gusa chini yake utaona machaguo ya mtandao yenye kumanisha aina ya mtandao wa internet.
Chagua:
  • GSM only kwa 2G peke yake
  • WCDMA only kwa 3G peke yake
  • LTE only kwa 4G peke yake


ZINGATIA HAYA:

Njia hii inafanya kazi kwenye simu nyingi za android lakini baadhi ya smartphones kama Samsung inakataa. Hivyo kama una simu ya jinsi hii na unatumia Android fanya rahisi ifuatavyo:

  • Nenda kwenye Settings za simu
  • Angalia kipengele cha Network
  • Chagua Mobile network
  • Bofya Network mode
  • Yatatokea machaguo ya mitandao ya internet kulingana na uwezo wa simu yako yaani 2G, 3G, na 4G.

KWA SMARTPHONE ZINAZOTUMIA WINDOW

  • Nenda sehemu ya kupigia simu
  • Bonyeza ##3282 au ##3282#
  • Bofya kwenye kwenye […] vidoti 3
  • Kisha chagua mtandao unaotaka kufanya simu yako iutumie muda wote yaani >> 2G, 3G, au 4G.
Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 Maoni :

  1. CASINOS - JTG Hospitality
    JTG Hospitality offers the latest in innovative and innovative 경주 출장샵 casino 서울특별 출장마사지 games including slots, table games, bingo, video slots, 서산 출장안마 and video  Rating: 4 나주 출장안마 · ‎1 대구광역 출장샵 review

    ReplyDelete