Unaweza badili kila USB port na ikawa si suruhisho, unaweza zima kompyuta yako na kuwasha au Kuformat hiyo memory pia ikakusumbua na usipate jibu, Kwa kuwa umetembelea kurasa zangu basi ondoa shaka tatizo lako limekwisha na wala usitupe na kununua Memory nyingine na kudhani kuwa wadudu "Virus" wameshaishambulia Memory yako. Hebu soma hatua zifuatazo jinsi ya kufanya:
1. Ingiza Memory yako kwenye Kompyuta
2. Fungua CMD "Command prompt" (Kama window 7, bonyeza "start" kisha andika "CMD" Sehemu ya kutafuta "search")
3. Baada ya ubao mweusi kufunguka
4. Andika diskpart Kisha Bonyeza "Enter"
5. Andika list disk Kisha Bonyeza "Enter"
6. Andika select disk x (x ni herufi ambayo imechukuliwa na memory yako uliyoweka kwenye kompyuta) Kisha Bonyeza "Enter"
7. Andika clean Kisha Bonyeza "Enter"
8. Andika create partition primary Kisha Bonyeza "Enter"
Sasa unaweza kwenda kwenye "disk management" na Kisha kuifomat Memory yako.
Na itakuwa tayari kusoma 8GB
* Kama hufaham kufomat memory yako kwa kuingia kwenye "disk management" tafadhari Andika Comment yako,au tuma mail kwa kubonyeza link ya hapo chini upande wa kulia ili nikusaidie zaidi * Asante...
0 Maoni :
Post a Comment