OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

Je, Umefuta IMEI kwa bahati mbaya kwenye Simu yako? Usijari unaweza kuirudisha sasa. Soma hapa

Imei ni kitu cha msingi sana kwenye simu yako maana ndio inakusaidia wewe kuweza kupata mawasiliano. Endapo simu yako itapoteza Imei zake basi utajikuta simu yako haiwezi kupata mawasiliano yeyote.


Simu nyingi za android huwa zinakumbana na tatizo la kupoteza au kufuta imie pale unapo factory reset au unapoweka custom rom. Leo tutajifunza njia itakayo kusaidia kuweka Imei kwa kutumia computer kwenye zile simu ambazo zimepoteza Imei. Njia hii imeajaribiwa kwenye simu ya android (SONY X-BO V3+) kama inavyo onekana kwenye picha chini .




Njia hii inafanya kazi kwenye simu zote zinazotumia MTK (MediaTek Processor) kama Vivo, Tecno, Huawei(baadhi), HTC (baadhi) etc.

Tahadhari

USITUMIE HII NJIA KUBADILISHA IMEI KWENYE SIMU AMBAZO ZIMEFUNGIWA KUTOKANA NI FAKE, UTAFUNGWA. MIMI SITAHUSIKIA ENDAPO UTAVUNJA SHERIA ZA TCRA TANZANIA. TUMIA HII NJIA KUJIFUNZA NA SIO KUVUNJA SHERIA.


Vigezo na Masharti 

0: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako
1: Hakikisha simu yako inatumia mtk (MediaTek Processor)
2: Computer inayotumia windows
3: Hakikisha umeweka vcom driver kwenye computer yako
4: Hakikisha tayari ume root simu yako

STEP 0 Hakikisha una computer inayotumia windows na tayari umeweka vcom driver kwenye computer yako. Kama bado tembelea link chini kujua jinsi ya kuweka vcom driver kwenye computer inayotumia windows
https://thebroodle.com/microsoft/windows/how-to-install-mtk65xx-preloader-usb-vcom-drivers-in-windows/
 
STEP 1 Download Mtk Droid Tools kwa kutumia link chini kisha extract kwenye computer yako.
https://mega.nz/#!1YhgFQQa!POGHsHKN2uA5B8uKCWk9F_YNDy0ej0oztxuUC2MWBhY
STEP 2 Ndani ya file ulilo download kwenye step 1, utaona mafile kama yanavyo onekana kwenye picha chini



STEP 3 Double click file linaloitwa MTKdroidTools.exe na utapata muonekano kama picha chini




STEP 4 Chomeka simu yako kwenye computer kwa kutumia USB Cable. Kwenye hili somo nimetumia simu aina ya (SONY X-BO V3+). Endapo utafanikiwa utapata muonekano kama picha chini.




STEP 5 Bonyeza sehemu iliyoandikwa Root kama inavyo onekana kwenye picha chini




Endapo utapata ujumbe kama picha chini basi bonyeza YES




STEP 6 Baada ya kubonyeza Root utapata maneno yanaosema root shell it is received temporarily before reboot. Kama hujapata maneno basi rudia upya maelekezo. Endapo utafanikiwa utapa muonekano kama picha chini




STEP 7 Bonyeza kipengele kilicho andikiwa IMIE/NVRAM kama inavyo onekana kwenye picha chini




STEP 8 Utapata kibox ambacho kinakwambia ujaze IMIE 1 pamoja na IMIE 1 kama picha inavyo onekana chini. Kama simu yako ni line mbili basi jaza Imie unazotaka kuweka kwenye simu yako. Kama simu yako ni line moja basi utapata kibox kimoja. Baada ya kuandika Imie zako, pembeni bonyeza kipengele kinachosema Replace Imie, Kisha bonyeza YES kisha bonyeza ok.

STEP 9 Bonyeza kipengele kinachosema Reboot kama inavyo onekana kwenye picha chini




Simu yako itajizima na kujiwasha. Baada ya hapo utakuwa umefanikiwa kurudisha au kubadili Imie. Ili kuhakiki kama imie zako zimebadilika basi piga number *#06#

Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Maoni :

Post a Comment