BIOS password hutumika kuongeza ulinzi wa ziada kwenye Kompyuta yako. Unaweza kuweka Password kuzuia mtu kuto ingia kwenye system BIOS au kufanya Booting ya PC.
Lakina wakati mwingine Ulinzi huo wa ziada unaweza ukakusababishia maumivu pale unaposahau BIOS password au kama mtu amebadili System BIOS kutoka mpangilio wake.
Lakini ondoa shaka, Kuna njia nyingi zinazofahamika za ku reset/kuondoa Password:
1. Kwa kuondoa CMOS betri
2. Kwa kutumia jumper za Motherboard
3. Kwa kutumia MS DOS command
4. Kwa kutumia Programu
5. Kwa kutumia Backdoor Bios password
Sasa nitajitahidi kuelezea kila njia tajwa hapo juu:
ILANI: Maelezo hayo ni kwa msaada wa watumiaji wa kawaida. Na si kwa matumizi ya wizi au maovu yeyote katika utumiaji wa kompyuta.Tafadhari usifanye nje ya taratibu na sheria za ICT na usifanye endapo huna uzoefu na Kompyuta. Siyo kwamba usitumie maelezo hayo, tumia endapo unajua na unauzoefu na kompyuta, kwa kuwa unaweza ukaharibu kabisa kompyuta yako au kupoteza Dta zako zote.
1. Kwa kuondoa CMOS betri
Kwa Motherboard zote daima hutumia kasarafu kadogo cheupe ambayo ni CMOS betri ili kutunza BIOS settings zote ikiwemo password. Ku reset password, Chomoa wire za PC, Fungua kasha lake na ondoa CMOS betri kwa makadilio ya dakika 15-30 na kisha irudishe tena. Ita reset setting zote za BIOS na ikiwemo password na unahitajika kuingiza tena upya setting zote.
Kama itashindwa, basi jaribu kuondoa betri kwa muda wa saa moja
2. Kwa kutumia jumper za Motherboard
Kwa kawaida Motherboard huwa zinakuwa na jumper ambayo inaweza kufura CMOS settings zote kwenye BIOS password. Sehemu iliko jumper inategemea na toleo la Motherboard. Unatakiwa kusoma Manual ya motherboard yako na kuangalia jumper zilipo. Kama huna Manual basi angalia jumper jirani mwa COMOS betri. Watengenezaji wengi wana lebo jumper kama CLR, CLEAR, CLEAR CMOS, n.k
Unapoipata jumper, angalia kwa makini. Itakuwa na pin 3. Na jumple huwa inaunganisha upande wa kulia na kushoto. Sasa unatakiwa ufanye nini, ni kuondoa jumper na kuunganisha na pin ya kati na pin ya pembeni yake. Kwa mfano kama jumper imechomekwa kwenye pin ya kati na kushoto, kisha ondoa hapo na uweke ya kati nay a kulia. Sasa subiri kwa muda mchache na kisha ondoa tena jumper na uweke tena pin ya kati na kushoto.
Hakikisha kuzima PC yako kabla hujafungua kasha lake na ku reset hizo jumper
3. Kwa kutumia MS DOS command
Njia hii inafanya kazi tu, kama una access ya system inapowashwa, kwasababu njia hii inahitaji MS DOS.
Fungua Command prompt kutoka kwenye program Menu na weka command moja baada ya moja:
debug
o 70 2E
o 71 FF
quit
Note: Herufi ya kwanza kwenye hizo command za hapo juu ni English alphabet “o” na siyo namba 0
Baada ya kuweka command hizo, restart system yako na ita reset CMOS Setting kwenye BIOS password.
Ngoja nikueleze kidogo kuhusu hizo commnd za hapo juu;
Kwenye njia hii tunatumia Debug tool ya MS DOS. Herufi “o” inakuwepo katika ya kwanza kwenye hizo command
Output thamani kwenye IO ports, namba 70 na 71 ni namba za port ambazo zinatumka ku access CMOS memory. Kwa kuweka thamani ya FF tunaiambia CMOS kwamba kuna invalid checksum na reset CMOS setting ikiwemo BIOS password.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 Maoni :
Post a Comment