*Ni vizuri kusherehekea mafanikio lakini ni muhimu zaidi kukumbuka uliposhindwa awali***.
*Usijifananishe na mtu yeyote katika dunia hii, ukifanya hivyo utakuwa umejitukana mwenyewe**
Bill Gates - (William Henry Gates III) Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, mtu tajiri sana duniani na mwanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
Bill Gates ni mwanzilishi, mwenyekiti na mbinifu mkuu wa programu za kampuni ya ya Microsoft, kampuni ya programu yenye mafanikio zaidi duniani, inayoaminika kwa utengenezaji wa programu zilizo na nguvu na ubunifu hali zikiwa bado zenye utumizi mwepesi. Microsoft sasa inaajiri zaidi ya watu elfu hamsini na tano katika nchi themanini na tano.
William Gates III H anajulikana kama Bill Gates alizaliwa tarehe 28 Oktoba 1955 na kulelewa katika kijiji cha Seattle pamoja na dada zake wawili. Katika umri wake mdogo Bill Gates alivutiwa na utengenezaji wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini Seattle. Akiwa huko shuleni Seattle, Bill Gates alikutana na Paul Allen, mwanafunzi mwenzake wakawa marafiki. Hapo ndipo wakaanza kutumia tarakilishi ndogo ya shule kujiendeleza ujuzi wao.
Waliajiunga na kampuni ya kompyuta, malipo yao ikiwa ni kutumia tarakilishi yenye nguvu zaidi. Kazi yao ilikuwa ni kutafuta nukshi katika mitambo ya kompyuta, wakati huohuo waliweza kijifunza lugha mpya za kompyuta. Bill akaenda kwenye Chuo Kikuu cha Harvard. Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paulo kuandika toleo jipya la programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair 8800.Kampuni hiyo iliridhishwa na kazi ambayo Bill Gates na Paul Allen waliofanya na programu hiyo ikapewa leseni. Jambo hili liliwachangia Gates na Allen Kuanzisha kampuni ya Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea kampuni zingine programu. Bill Gates aliacha masomo yake katika chuo kikuu cha Harvard na kujishughulisha muda wake wote katika biashara.
Mapumziko yao yalikuja walipotengeneza mfumo wa kuendesha kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika katika kompyuta ya kwanza ya kibinafsi ya IBM. Baadaye waliweza kuzishawishi kampuni zingine zinazotengeneza kompyuta kutumia mfumo huo wa MS-DOS. Mfumo huu mpya wa MS-DOS ulipata umaarufu katika soko miaka ya 1980 na baadaye, Microsoft pia ilianza kutengeneza programu kama vile neno sindikizi.
Microsoft ilitangaza mfumo mpya wa uendeshaji wa kompyuta uitwao Windows 1.0 mwaka wa 1983, ambao ulikuwa na grafiksi bora na pia uliwezesha kufanya zaidi ya jambo moja kwa wakati mmoja. Hata hivyo hakuwa bidhaa nyingine iliyotolewa miaka mbili baadaye hadi mwaka wa 1985, kwa kuwa ni programu chache zilizoweza kuendeshwa katika mfumo huu wa Windows 1.0. Hivyo mfumo huu mpya haukupata umaarufu vile.
Kipindi cha miaka mitano baadaye Microsoft ilitoa mifumo mipya ya Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi kuliko mifumo ya hapo awali. Kampuni ya Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi katika soko la hisa, na akiwa umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa bilionea mchanga zaidi katika historia ya Marekani.
Katika mwaka wa 1990 Microsoft ikiongozwa na Bill Gates ilitoa toleo jipya la Windows liitwayo Windows 3.0 na kuboreshwa kiasi GUI. Toleo hili jipya liliweza kuuzwa zaidi ya nakala milioni kumi, likifuatiwa na matoleo mengine ya Windows 3.1, 3.11 na makundi ya kazi ambayo yaliongeza misaada kwa mitandao. Kutokana na mafanikio yao ya maendeleo, Microsoft ilitoa matoleo mengine ya Windows 95 ikifuatiwa na Windows 98, 2000, Millennium Edition na toleo la sasa Windows XP. Kila toleo jipya lilipotolea kampuni ya Microsoft ilizidi kupata umaarufu katika soko la hisa, ikiongezwa na baadhi ya programu kama vile Microsoft Office, michezo n.k. Umaarufu huu umemfanya Bill Gates kuwa mtu tajiri duniani myenye thamani ya wastani wa dola bilioni arubaini na sita.
Bill Gates pia ana maslahi katika biashara nyingine akiwa na nafasi nyingi za uwekezaji na vyeo katika kampuni tofauti ikiwemo Corbis Corporation, Berkshire Hathaway Inc, Teledesic Corporation. Mwaka wa 1998 Gates alijitoa jukumu lake kama Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Microsoft na kuzingatia maendeleo ya teknolojia na bidhaa mpya.
Bill Gates alifanya ndoa na Melinda French Gates mwaka wa 1994 na wakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na Fibi. Wote wawili Bill na Melinda ni waanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Waliweza kulianzisha shirika la Bill na Melinda Gates Foundation ambalo limeweza kuchangia zaidi ya dola bilioni tatu nukta mbili kuboresha afya duniani, dola bilioni mbili kuboresha fursa ya masomo kwa familia zisizojiweza. Zaidi ya hayo limeweza pia kuchangia dola milioni mia nne sabini na saba kwa miradi ya jamii na zaidi ya dola milioni mia nne themanini na nane kwa miradi maalum na kampeni za kuhamasisihwa kila mwaka.
Ubunifu wa Bill Gates wa kutengeneza programu umekuwa mchango wake katika mapinduzi ya kompyuta na sayansi ya kompyuta.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 Maoni :
Post a Comment