OFA!! OFA!! - PATA MSAADA KWA WATAALAMU WA IT BURE, TEMBELEA TUVUTI KWA KUBONYEZA HAPA AU WHATSAPP: +255678 920112
News
Loading...

IJUE KOMPYUTA [SEHEMU YA PILI] (Jifunze hapa Mambo mengi Kuhusu Kompyuta ni BURE)



NI VIPI WATU WANAIBIWA TAARIFA ZAO KWA SABABU YA KUUZA KOMPYUTA ZAO BILA KUSAFISHA?

Kuna watu wamekuwa wakipata hasara katika makampuni yao au hata watu binafsi kutokana na kuuza kompyuta zao kwa watu wengine .Uuzaji wa kompyuta bila kuisafisha umeawafanya watu wengi kuibiwa kumbukumbu zao za siri bila wao kufahamu na kumbukumbu hizo zinapoangukia kwenye mikono ya watu wabaya inakuwa hasara kwa aliyeuza kompyuta hiyo.JeUnataka kuuza kompyuta yako na kununua mpya,lakini kwenye kompyuta yako kuna kumbukumbu nyingi za muhimu ambazo usingependa mtu mwingine yeyote azipate wala kuziona.Je utafanya nini?

Wapo ambao wamekuwa wakitumia mbinu za kawaida kufuta data kwenye kompyuta zao kama Kufuta(delete) au kuformat .Utafuta kila kitu kwa kubonyeza "Delete" halafu kwenda jalala(Recycle bin) kufuta kila kitu Au utaamua kuformat na kuifanya kompyuta yako kufuta kila kitu.Hii Haitasaidia Swali ni je njia ipi ni sahihi ya kusafisha kompyuta yako kabla ya kuiuza?

Majibu ni mengi na inategemea na ufahamu wa muhusika,ila ukweli ni kuwa kwa njia zote mbili za hapo juu hakuna hata njia moja iliyo salama,kwani kama utatumia njia kama hizo na ukamuuzia
mtu mwenye utaalam wa kompyuta,basi ataweza kuzirudisha(recover) kumbukumbu zote ambazo mwenyewe ilizani zimefutika.Kbla ya kujua njia za kujikinga basi tuone ni kwa namna gani kompyuta inatunza kumbukumbu.

Jinsi kompyuta inavyohifadhi kumbukumbu
Wengi wetu wanaweza wakawa wameshaanza kujiuliza,inakuwaje sio salama wakati nimeshafuta kila kitu toka kwenye kompyuta? Je mtu ataweza vipi kuona mafaili ambayo tayari nimeshayafuta?
Ukweli ni kuwa,kwa mujibu wa uhifadhi wa kumbukumbu kwenye kompyuta.Pindi unapofuta au kufanya format(kuweka mtambo endeshi(OS) mpya),sio kweli unayafuta moja kwa moja mafaili na kumbukumbu
toka kwenye kompyuta yako.Kitu kinachofanyika ni kuwa unaondoa taswira yake kwenye uso wa mbele wa hard disk hivyo kukufanya wewe uone kama umeyafuta ila bado yanaendelea kuwepo kwenye disk yako.Na hii ndio maana kama kunatokea kesi,wataalam wa uchunguzi wa makosa ya kompyuta(Computer Forensic) huchukua kompyuta yako kwa ajili ya kuifanyia uchunguzi.

Siku hizi kuna program nyingi sana ambazo zina uwezo wa kurudisha mafaili hata yale yaliyokuwepo kipindi ulipoinunua kompyuta kwa siku ya kwanza, mara nyingi jinsi gani unaweza kuyarudisha
hayo mafaili hutegemea elimu ya mtu anayefanya hizo kazi ya kuyarudisha,kwani kazi ya kuyarudisha haya mafaili huwa ngumu kutegemeana na jinsi mafaili hayo yalivyofutwa.Mfano faili
lililofutwa kwa kubonyeza "Delete" ni rahisi zaidi kulirudisha kuliko lile lililofutwa kwa kuformat kopyuta, vilevile huwa ngumu zaidi kama mtumiajai alifanya mgawanyo wa hard disk (partition) baada ya kuformat.
Hivyo leo hii nitakuonehsha njia thabiti za kufuta kumbukumbu toka kwenye kompyuta unayotaka kuiuza ili kuhakikisha unakuwa salama zaidi.

Nitafutaje kumbukumbu moja kwa moja toka kwenye kompyuta?
Takwimu zinaonesha kuwa mtu mmoja kati ya wanne wamekuwa wakiibiwa siri zao kutokana na kuuza kompyuta bila kufuta kumbukumbu,hivyo kama wewe hutaki kuingia kwenye hilo kundi basi unaweza kufuata hatua zifuatazo.
1.Chukua ile CD uliyopewa pindi uliponunua kompyuta yako,ambapo nyingi huitwa recovery CD.Kama umepoteza hii CD au haukupewa pindi uliponunua kompyuta,basi nenda online na tafuta programu zinazotumika kufuta kumbukumbu(disk-wiping program). Programu hizi zipo nyingi ila binafsi nimewahi kutumia Darik's Boot and Nuke (DBAN) hivyo nakushauri uijaribu hii.

2.Tumia programu kama Nero au yoyote uliyoizoea kuchoma hayo mafaili ya hii programu kwenye CD,kumbuka kuchagua mtindo wa Bootable CD.

3.Weka CD kwenye kompyuta yako halafu irestart. Kompyuta inatakiwa kuitambua hiyo CD pindi tu inapowaka,kutatokea ujumbe kwenye kioo unaosomeka "press any key to boot from CD." Hapo bonyeza kitu chochote kwenye keyboard yako.

Kumbuka: Kama hautouona huu ujumbe unaosomeka"boot from CD" inawezekanika kabisa umekosea katika kuchoma hiyo CD yako,unatakiwa kuichoka kama "Bootable CD".

Jaribu tena au wasiliana na mtaalamu wa IT aliye karibu nawe. Kama una uhakika kabisa uliichoma kama Bootable CD,basi inawezekana kuna mabadiliko unatakiwa kuyafanya ili kuiwezesha kompyuta kuitambua CD,haya kwa wasio na utaalam inabidi wawatafute wenye utaalam kidogo ili wakusaidie kubadilisha utaratibu wa BIOS.

Kama unataka kujaribu mwenyewe,basi kompyuta inapowaka tu bonyeza "Delete",baada ya hapo fuata maelekezo na kuingia kwenye "Boot Sequence",iweke CD or DVD kuwa ya juu kabisa kabla ya Hard drive,hapo mambo yatakuwa sawia.

4.Fuata maelekezo utakayopewa na hiyo programu,mara nyingi huchukua masaa kadhaa hadi siku mpaka kufuta kila kitu kilichopo kwenye kompyuta yako.
Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto.

Baada ya hapo basi kompyuta yako itakuwa mbichi kabisa na unaweza kuiuza bila utata wala hofu juu ya kumbukumbuku wala usalama wako.

Unajua umuhimu wa teknolojia ya kompyuta? 
wapo watu ambao kwa namna moja au nyingine wanaona kuwa hamna umuhimu wa mtu kumiliki kompyuta ,au hata kujifunza kuijua kompyuta .Wapo wengine ambao wanaona kompyuta ni kama kitu fulani cha anasa na hivyo hakina umuhimu,hii sio kweli hasa katika dunia hii ya leo ya sayansi na teknolojia ,kompyuta ni kitu cha msingi sana kuwa nacho au kuwa na umuhimu katika kukitumia ,katika safu hii leo tutachambua faida za kuwa na kompyuta ,kwa kuangalia hasa matumizi ya kompyuta na hivyo baada ya kusoma habari hii utapaswa kujiuliza kuwa kama kuna umuhimu wa kuwa na computer au la.

Je kuna umuhimu gani kama wewe na mimi pekee tukijua matumizi ya teknolojia ya sasa na kuwahacha watu wengi ususani vijana wakiwa bado wako nyuma katika matumizi ya kompyuta,kama ukiangalia vijana wengi
wa sasa wanajua nini maana ya computer lakini hawajui matumiziyake,wengi wanaishia kuangalia picha za ngono na kuskiliza miziki,na wanaofanya vitendo hivyo wengi wao na wanafunzi,nimejaribu kuchunguza huu sasa ni mwezi wa sita na jibu nililopata kwamba vijana vijanawengi wanaopoteza muda wao kwa kuangalia vityu vya kipumbavu wengi wao ni wanafunzi wa shule za secondary na vyuo .

Kompyuta ama kibwebwezo ni mashine yenye mfumo ulioundwa na muunganiko wa maunzi (hardware) au vifaa vinavyofanya kazi kwa pamoja kupokea data, kuchakacha (process), kuzihifadhi na kuzitoa kwa matumizi mbalimbali. Hii ni mashine ya kielectronic inayofanya kazi mbalimbali ambazo zingechukua muda kufanywa na binadamu.

http://ictyetu.blogspot.com/p/ijue-kompyuta-sehemu-ya-pili-inaendelea.html


Shiriki(Share) kwenye Google Plus

About ICT yetu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Maoni :

Post a Comment