Kompyuta ni mashine inayotumia data kwa njia tofauti kutokana na maagizo zilizoandikwa kwenye bidhaa pepe ( software). hivyo basi Kompyuta ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wa kupokea na kukusanya taarifa (Data), kufanyia kazi na kutoa matokea ya kazi hiyo na namna ilivyoendeshwa, pamoja na kutoa matokeo ya kitu kilichofanyika, yaani kinachoonekana (Information).
Teknolojia hii ni mabadiliko ya kisayansi yaliyowekwa kwenye nadharia ya utendaji kazi. Mabadiliko hayo yanapochochewa kwa kiasi kikubwa huwezesha mambo mbalimbali kuvumbuliwa na kuweza kuboresha shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na hata mawasiliano.
Kompyuta ni moja kati ya nyenzo zilizotokana na mabadiliko ya teknolojia ya hali ya juu
Aina za kompyuta
Kuna aina kuu tatu za kompyuta, nazo ni kama ifuatavyo:-
1. Digital Computers: Ni kompyuta zinazotumika kwa ajili ya kufanyia hesabu pamoja na kazi za kutumia akili.Kompyuta za aina hii ndio ambazo zipo katika matumizi hasa katika Dunia hii ya mabadiliko ya teknolojia.
2. Analog Computers:
Ni kompyuta zinazotumika kwa ajili ya kupokea taarifa (Data) kama zile za kusomea hali ya hewa, kupimia mishipa ya damu na kupimia kiwango cha chumvi kwenye maji.
3. Hybrid Computers:
Kompyuta hizi zinafanana na zile zilizotangulia kutajwa hapo mwanzo, nazo zinatumika kwa ajili ya kutafutia taarifa (Data) kutoka kwa binadamu moja kwa moja na kupitia mandishi na vipimo.
Aina za digital kompyuta
Super Computers:
Takriban zinapatikana sehemu zote duniani, na zinauwezo na nafasi kubwa ya kuhifadhi vitu vingi (Information) na zinatumika kwa ajili ya kazi za kijeshi na sehemu za ukaguzi, pia kompyuta hizi haziruhusiwi kuhamishwa nje ya nchi na kujua jinsi gani zinatumika. Na zinasifika kuwa na umbile la kati na kati, pia zina uwezo mkubwa na uwepesi wa hali ya juu.
Mainframe Computers:
Nazo ni kompyuta zenye umbile kubwa, na zilianza kudhihiri kwake katika mwanzo wa miaka ya hamsini, nazinasifika kwa uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu na pia uwepesi wa hali ya juu.
Mini Computers:
Aina hizi za kompyuta zilidhihiri katika kipindi cha miaka ya sitini.Ni kompyuta zenye umbile dogo kuliko zile zilizotangulia kutajwa,na ni bora kwa kuunganishia kompyuta nyengine zinazotumika viwandani na ndani ya nchi.
Micro Computers:
Aina hii ya kompyuta inakusanya aina zifuatazo:-
Personal Computers (PCs) ambazo ni maalumu kwa ajili ya matumizi ya mtu mmoja tu. Home Computers, Portable Computers: Nazo ni kompyuta za kubeba mkononi, ambazo zimegawanyika katika aina zifuatazo:-
1. Laptop.
2. Notebook.
3. Palmtop.
0 Maoni :
Post a Comment