Baadhi ya utatuzi huo unahitaji kufanya kama ufuatao:
HATUA 1:
Zima kompyuta yako na chomoa kila kilicho chomekwa. Kama unatumia Laptop, toa beti lake. Bonyeza Swich ya kuwashia bila kuachia kwa muda wa sekunde 15 hadi 20 au zaidi ili kufuta vyanzo vyote vya umeme vilivyoingia kwenye kompyuta yako. Baadhi ya swich za kuwashia za komputa huwa zinasambaza umeme kwenye kioo (screen) na kusababisha kuchemka kufanya kazi yake kama inavyotakiwa. Rudishia tena vitu vyote ulivyochomoa kihusahihi, kasha washa tena uone kama mistari imeondoka.
HATUA YA 2:
Chomoa waya wa picha wa kioo (screen) na usubiri mpaka itakapo onesha meseji kuwa “No signal”. Kama hakuna meseji nab ado inaonesha mistari iliyosimama basi tambua kuwa tatizo ni la kioo chako (screen) na siyo kompyuta. Bonyeza kitufe cha “Menu” kwenye kioo (screen) na kasha tumia vitufe vingine ili kuonesha modi ya “Factory setting”. Chagua hiyo modi ili kurekebisha kioo chako kiwe kama awali uliponunua dukani. Kama mistari bado basi kioo kinaweza kuwa kina poteza usumaku ambao huwezi ukaurekebisha, zaidi ya kununua kioo kipya.
HATUA YA 3:
Rudishia tena vitu ulivyochomoa kasha unapoiwasha kompyuta yako kama utaona hiyo mistari kabla hata Window yako haikuyaleta mafaili, basi tatizo yaweza kuwa ni kadi ya picha “VGA card”. Kama mistari inajitokeza baada ya window kuonesha mafaili yake basi tatizo lipo kwenye mpangilio wa Window yako (Screen Resolution). Bonyeza “Advanced Setting”, “Monotor” na pia refresh rate kama hiyo mistari inaweza potea.
TAZAMA VIDEO HII FUPI KWA MSAADA ZAIDI:
*Kama unahitaji msaada zaidi tafadhari usiache kukoment lolote hapo chini ili nikusaidie zaidi, Asante *
0 Maoni :
Post a Comment