Kama una kompyuta aina ya dell na haitaki kuwa na kuishia kuwaka tu taa ya rangi ya chungwa, basi itakuwa na tatizo la usambazaji wa nguvu ya umeme (power supply). Wakati mwingi sana hilo tatizo la kuwaka kwa flash taa rangi ya chungwa huwa linatokea mara kwa mara kwa tatizo la “Power supply”
Kuna hatua za kufanya ili kuweza kutatua hilo tatizo:
(Chomoa kebo zote za umeme)
1. Fungua Kasha la kompyuta yako ya Dell
2. Fungua box ya “Power supply” na utafute waya rangi ya kijani (Waya rangi ya kijani ndio unaotumika kama swichi ya kuwashia “Power supply” kwenye Kompyuta zote)
3. Ukate sehemu ya kati
4. Chuna kava yake sehemu zote za mwisho, ili upate waya wa ndani sehemu zote mblili za ulizokata
5. Tafuta kipande kingine cha waya mrefu ambao hakikisha unaweza fika sehemu ya mbele ya kompyuta yako
6. Chomea na waya wako wa kijani lakini weka tofauti na kipande chako cha waya
7. Zipange vizuri na uzifunge (kama kuna mkanda wake basi uzifunge vizuri)
8. Chomeka “Power cable” waya wa moto kwenye komputa yako
9. Pitisha waya wako kwenye makalio “Chassis” za kompyuta
10. Kama feni inawaka “full speed”, bonyeza kitufe cha kuwashia “Power button” na toa waya wako “Put off”
11. Sasa Kompyuta yako itawaka kama kawaida..
· Tafadhari kama hukuelewa usiache acha Comment yako ili nikusaidie zaidi *
Sijaelewa bado nipitishe kwenye chassis ya computer kuelekea wapi
ReplyDeleteLaptop aina ya dell ni kiunganishi waya wa adapter taa ya betri inawaka kama indicator rangi ya orange na haipeleki moto.Msaada Tafadhari
ReplyDeletepc dell inawaka wakati wa kudisplay neon dell inazima gafla ukirudia kuwasha inawaka ila inaonyesha automatic repair shida itakuwa n nn?
ReplyDeleteHabari samahan laptop yangu niliifungua kurekebisha speaker sasa kilichotokea ni kwamba nikiiwasha sasa hivi kioo hakipati moto yaan hakiwaki na ile power button nikibonyeza inawaka na kuzima na nikieka chaji taa ya umeme inawak kma sekundi 5 nakuzima kioo hakiwaki kbsa sijajua taxo ni nini?
ReplyDeletePc yangu aina ya dell imezima ghafla, lakini nilipo jaribu kutoa betri na kuirudisha tena caps lock ikawaka na kuzima, lakini hadi sasa kitufe cha kuwashia kinakua on hata kama sijaiwasha na haionyeshi kitu. Msaada kwa anae jua nini laweza kua tatizo
ReplyDeleteJamani naomba msaada PC yangu Aina ya Dell Ina Waka nakujizima Ina onesha Kama inawaka alafu inakata Moto nifanyeje wakubwa?
ReplyDeleteNa je vipi kwa hp yamlalo inawaka taa nyekundu
ReplyDelete